Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 29,2014 SAA 10:57 JIONI
Mshambuliaji wa Ubelgiji
Romelu Lukaku amesema kuwa klabu
Chelsea ndio watakao toa "neno la mwisho" juu ya kujadiliwa mustakabali wake msimu huu .
Chelsea ndio watakao toa "neno la mwisho" juu ya kujadiliwa mustakabali wake msimu huu .
Mchezaji huyo anacheza kwa mkopo katika klabu ya Everton na ana mabao 13
katika mechi 29 lakini bado haijafahamika juu ya matarajio yake ya baadaye .
Lukaku aliiongoza Ubelgiji kufika katika fainali za Kombe la Dunia
2014 , ambayo itaanza katika Group H katika mashindano hayo, dhidi ya timu ya Algeria,
Russia na Korea ya Kusini.
Mchezo mzuri katika michuano hiyo ya kuelekea Brazil kulichochea kuongeza uvumi juu ya uhamisho wa mchezaji huyo, lakini mchezaji huyo mwenye 6ft 3ins amesema kwa sasa anazingatia Ratiba ya mwisho wa Ligi ya klabu ya Everton ,ambapo wakiwa nyumbani watawakaribisha Manchester City siku ya Jumamosi jioni
na pia watacheza na Hull City wiki inayofuata siku ya Jumapili.
Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, Lukaku aliiambia Het Nieuwsblad: "tutaona mwishoni mwa msimu,kwa sasa mimi nina lenga kufanya vizuri katika klabu ya Everton".
"Mimi bado nina mkataba mpaka 2016 katika klabu ya Chelsea na nadhani wao wana furaha kwa jinsi ninavyofanya vizuri"
"Wao watakuwa na neno la mwisho, hivyo tutaona nini kinatokea siku zijazo."
Lukaku kwa sasa yuko katika chati ya wafungaji 10 wa Ligi Kuu ,katika ngazi na mchezaji wa Liverpool Steven Gerrard na wa Newcastle Loic Remy.
Katika msimu uliopita,alifunga mara 17 akiwa kwa mkopo katika klabu ya West
Brom, aliingia mara sita katika mbio kugombea kiatu cha dhahabu na alikuwa ameshinda tuzo ya Mwaka ya mchezaji anayechipukia katika chama cha soka cha PFA .
0 Comments