Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 24,2014 SAA 09:16 ALFAJIRI
Bosi wa Bayern Munich Pep Guardiola amejivunia timu yake,
licha ya kufungwa 1-0 na Real Madrid katika mechi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya nusu fainali.
Mabingwa hao wa Bundesliga waliongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 72 ya mchezo zaidi ya dakika 90 - lakini hawakuweza kushinda,kwani bao la Karim Benzema katika kipindi cha kwanza lilionekana kuleta utofauti.
"Najivunia timu yangu," alikiambia kituo cha utangazaji cha Ujerumani ZDF.
"Wamepambana vizuri dhidi ya mpinzani wagumu, na ni moja ya timu bora duniani. Tulikuwa tuna cheza vizuri na natumaini tutafanya maboresho zaidi wiki ijayo".
Ronaldo ambaye alimpisha Gareth Bale ambaye aliripotiwa kuukosa mchezo huo kwa sababu ya kuugua mafua, na Angel Di Maria wote walipata nafasi nzuri za kukabiliana na mashambulizi ya Bayern,na nahodha wa Bayern Philipp Lahm alikiri kwamba yeye na wachezaji wenzake walikuwa hawawezi kushughulikia kasi ya Real.
"Tuache yote, Real walikuwa haraka baada ya mapumziko," alisema Lahm. "Wao ni timu ya juu. Haiwezekani waache nafasi angalau moja. Sisi tulicheza ili kushinda, tulitaka kushinda na Sasa tunatafuta kushinda ".
Kipa wa Bayern Manuel Peter Neuer pia aliunga mkono mawazo Lahm lakini alibakia kupinga kwamba wanaweza kutolewa timu hizo mbili zitakapokutana tena mjini Munich wiki ijayo.
0 Comments