Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 22,2014 SAA 06:50 USIKU
Mashabiki wa Manchester City wamewasisitiza wapinzani wao Manchester United kuwa hawapaswi kumtimua meneja
Vita vya panzi ni furaha kwa kunguru: mashabiki Manchester City wakishikilia bendera ya kumuombea David Muyes ambayo inasomeka'Msimfungie virago Moyes' (wakileta utani)
|
Kila mtu alikuwa na mawazo yake: 'David Moyes ni mtu wa Fikra ya soka', Shabiki wa City akileta utani |
Mashabiki hao walibeba mabango yaliyosomeka ' Usimfukuze Moyes' na lingine 'David Moyes: Football Genius' wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu na West Bromwich Albion siku ya Jumatatu usiku.
Mashabiki wa City wakionyeshwa ujumbe kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu na West Brom |
Taarifa zimeripotiwa kuwa Moyes ataachishwa kazi ya kuwa na Manchester United baada ya matokeo mabaya ya msimu wa kwanza wa malipo
|
Kuweka imani: City bado wako katika mbio za kutwaa ubingwa , lakini Liverpool wana nafasi kubwa.
|
Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa Moyes atatimuliwa katika klabu ya Manchester United katika kipindi cha wiki zinazokuja baada ya wamiliki wa Klabu ya United ,familia Glazer hatimaye wamepoteza uvumilivu na Mscot huyo ambaye aliteuliwa msimu uliopita baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson,na sababu pekee ya kupoteza matumaini na kocha huyo ni kufuatia msururu wa matokeo mabaya msimu huu.
Lakini Klabu ya Manchester United inasema kuwa David Moyes hajafutwa kazi na kukataa kuzungumzia mstakabali wa kocha huyo katika klabu hiyo.
Msemaji wa klabu hiyo alithibitisha kuwa Moyes bado hajafutwa kazi.
Alipohojiwa kuhusu ikiwa kocha huyo ataaga klabu hiyo kabla ya mwisho wa msimu,alijibu kwa kusema kawaida hawazungumzii utabiri.
Hata hivyo hakuna hata gazeti moja lililosema moja kwa moja kuwa Moyes amefutwa kazi.
Jarida la Daily Mail limenukuliwa likisema kuwa Moyes huenda akafutwa kazi kabla ya msimu kuisha wakati Daily Telegraph likisema amepoteza uungwaji mkono wa wamiliki wa klabu hiyo na huenda akafutwa kazi.
Moyes aliteuliwa na Sir Alex Ferguson, kumrithi kama meneja wa klabu hiyo alipostaafu baada ya kuhudumu kama meneja kwa miaka 26
Moyes mwenye umri wa miaka 50, alipewa mkataba wa miaka sita na kuondoka Everton kuongoza mabingwa wa ligi lakini mkataba wake huenda unaelekea ukingoni baada tu ya miezi kumi.
0 Comments