Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MBANGWA:WAYNE ROONEY MASHAKANI KUCHEZA MCHEZO WA PILI DHIDI YA BAYERN MUNICH

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 05,2014 SAA 08:09 USIKU
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney ana mashaka makubwa  kwa kutokuwepo katika mchezo wa robo fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano dhidi ya
Bayern Munich kwa sababu ya kuumia kidole cha mguu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ilikuwa msaada mkubwa katika siku ya Jumanne usiku katika mchezo ambao walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa wa tetezi wa taji la Ulaya.

Dhahiri atakosa safari ya mchezo wao dhidi ya Newcastle United siku ya Jumamosi na mshambuliaji mwenzake  Robin van Persie tayari yuko kando, hii ni habari mbaya kwa meneja David Moyes.

klabu iliweka ujumbe katika mtandao wao rasni waTwitter siku ya Ijumaa jioni: "imethibitishwa. Wayne Rooney anatarajia kukosa @ NUFC vs # mufc, anaweza kuwa na mashaka kwa ajili ya safari dhidi Bayern"

Moyes aliiambia MUTV.. "ameumia kidole,kimepondeka vibaya kidole, Si tu ni tatizo kwa mchezo huu, inaweza kuwa tatizo kwa ajili ya mechi Munich".

"Hatuna budi kufuatilia. Tutaweza kuwa naye katika matibabu ya mwishoni mwa wiki na kuona kama tunaweza tukawahi."
Ingawa Rooney amefunga mabao mawili tu ya Ligi ya Mabingwa msimu huu,kama atakuwa amekosa mchezo huu,atakuwa amekosa mchezo muhimu wa United ambao ni lazima washinde ili waweze kuendeleo na safari ya kulekea nusu fainali ya Ligi ya Mabangwa.

Post a Comment

0 Comments