Kocha wa Evarton Roberto Martinez amesema David Moyes
atarudisha matumaini katika maswala ya usimamizi wa mpira hivi karibuni.
Roberto Martinez aliletwa katika klabu hiyo wakati Moyes alipoelekea Manchester United na imesababisha timu ya Everton kuwa na ndoto za kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwa michezo yao mitatu ya msimu iliyobaki.
Baadhi ya mashabiki wa Everton wamemgeuka meneja wao wa zamani, ambaye alitumia miaka 11 na klabu hiyo na kuifanikisha kumaliza katika nafasi nne za juu mwaka 2005.
Lakini Martinez alisema: "Tunamtakia mafanikio bora, daima tuko pamoja naye kimawazo na sisi siku zote tunamshukuru kwa kazi aliyofanya katika klabu yetu".
"Ni si hali nzuri kwa meneja kupoteza kazi yake, hasa mtu ambaye aliiweka katika nafasi nzuri , na nguvu klabu yetu".
"Nina uhakika atakuwa tayari kupata kazi nyingine kwa haraka kama itawezekana na nina uhakika yeye hakuwa mkosefu kutoa fursa kwa mtu ambaye anafanya kazi ngumu, ana umakini na anajitolea katika kazi yake"
0 Comments