Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 08,2014 SAA 01:49 USIKU
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) imeendelea leo (Machi 8 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo
Coastal Union waliumana na
Ashanti United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
Na katika mchezo huo wenyeji Coastal Union wameshindwa kufurukuta baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana.
Ruvu
Shooting iliwakaribisha Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani
Pwania,na maafande hao wa Ruvu Shooting waliwachezesha gwaride maafande wenzao wa kuwafunga bao 1 kwa 0.
Na Mbeya City imeendeleza ubabe kwa kewatandika Rhino Rangers mabao 3 kwa 1,katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kesho Jumapili (Machi 9 mwaka huu) ni Tanzania Prisons na Simba kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, na JKT Ruvu na Mtibwa Sugar zitacheza
Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

0 Comments