Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 08,2014 SAA 06:06 MCHANA
Mario
Balotelli anarudi katika kikosi cha AC Milan kwa ajili ya mechi yao ya Serie A dhidi ya
Udinese siku ya leo Jumamosi baada
ya kupona kutokana na kuumia bega.
"Balotelli
yuko vizuri, bado anajisikia maumivu kidogo lakini anahitaji ya mazoezi ili kuwa pamoja.,"Kocha wa Milan Clarence Seedorf aliwaambia
waandishi wa habari siku ya Ijumaa.
Mshambuliaji
huyo wa Italia, ambaye amefunga mabao 10 katika mechi 18 msimu huu, amekosa
mechi mbili za mwasho za Milan baada ya kuondoka uwanja dakika 12 kutoka
mwisho katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao walifungwa 1-0 na Atletico Madrid mwezi uliopita.
Mshambuliaji huyo amekuwa katika utata zaidi baada ya kuchapisha picha yeye mwenyewe katika ukurasa wake wa Twitter akicheza mchezo wa table tennis, hivyo kuzua madai katika
vyombo vya habari vya nchini Italia kwamba alikuwa hachukulii kwa umakini kuumia kwake.
"Siko hapa kwa ajili ya kuwaambia watu jinsi ya kutumia njia za mawasiliano yao wenyewe," Seedorf alisema.
"Ki vipi unapata habari nchini Italia na kuwa na wasiwasi kwangu. Hili ni
jambo kama lasilo na maana. Ni nani anayejali ikiwa alicheza table
tennis? Alikuwa kwa saa sita kwa matibabu."
Vijana hao wa Seedorf wako katika nafasi ya 10 katika Serie A wakiwa na pointi 35, sita nyuma ya wapinzani
wao wa jadi Inter Milan,Wao watasafiri kwenda katika mji mkuu wa Hispania siku ya Jumanne kwa raundi ya pili ya hatua ya-16 bora kupambana na Atletico.

0 Comments