Ticker

6/recent/ticker-posts

SOMA ALICHOKISEMA JOSE MOURINHO BAADA YA MCHEZO WA JANA KWA WACHEZAJI FABREGAS NA DIEGO COSTA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Aug.19,2014 SAA 09:21  ALFAJIRI
Costa

Jose Mourinho anaamini Cesc Fabregas na Diego Costa wanaweza kuipeleka Chelsea katika kiwango cha juu baada
ya wachezaji hao waliosainiwa msimu huu kuonesha makali katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley siku ya jana Jumatatu usiku katika uwanja wa Turf Moor.

Chelsea ilishangaza baada ya kutoka nyuma kwa kufunga na mchezaji Scott Arfield  lakini kwa juhudi za Costa, Andre Schurrle na Branislav Ivanovic waligeuza matokeo hayo.
Mourinho anahisi kuwa uelekeo wa timu yake inavyocheza na akimwangazia Fabregas aliyekuwa nyota wa mchezo pamoja na mshambuliaji Costa, anasema kutakuwa na ushindani kwa klabu nyingine.

Alisema waliudhibiti mchezo na wakati mwingi walikuwa bora kwa mtindo waliocheza.


Lakini Jose Mourinho kwanza alimuezea Fabregas baada ya kuwa nyota wa mchezo huo " ni nyota wa mchezo kwa sababu kiukweli alikuwa ni mwalimu na alithibiti mchezo na kumuelekeza (Nemanja) Matic"
"Alithibiti kasi na ukubwa wa mchezo"
"Diego alifanya kitu muhimu sana kwetu ambapo ilifunga bao la kwanza. Harakati zake na mwingiliano na Eden (Hazard), Oscar na Schurrle ulikuwa mzuri sana, ingawa nasema  samahani kwa ajili yake, kwa sababu  ilikuwa ni penalti na kamwe ile haikuwa kadi ya njano. "
Costa alipewa KADI ya njano wakati alipoonekana akujiangusha kwa kipa wa Burney  Tom Heaton, na Mourinho anasema kuna haja ya kuwa mfumo maalum ambao utatathimini upya kadi ya njano.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments