Gary Neville amemuonya Louis van Gaal kwamba lazima ajifunze kutokana na makosa ya gharama kubwa iliyotumika
katika utawala uliopita wa Manchester United na kumtaka asiwe na"hofu ya kununua" kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Mchambuzi huyo wa michezo amesema klabu yake hiyo ya zamani wanahitaji kuongeza wachezaji katika kikosi kama wanahitaji kushindana na kupata heshima kubwa tena, lakini alitaka klabu hiyo uchukuwe tahadhari juu ya kupoteza mamilioni kwa kuwachukuwa aina wachezaji wasiofaa.
United walitumia £ 165million kwa kununua wachezaji kama Juan Mata na Marouane Fellaini katika siku tano za mwisho za dirisha la usajili - huku PSG tu ndio waliotumia zaidi barani Ulaya katika kipindi hicho - lakini Neville anahisi fedha nyingi mno zilitumika kwa United
Na anasema Van Gaal lazima afuate sera tofauti za uhamisho wa David Moyes, licha ya wafadhili wa klabu hiyo kutoa fedha zaidi kwa ajili ya kutumia.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments