Mshanbuliaji wa Barcelona Lionel Messi amevunja Rekodi ya mkongwe wa Real Madrid, Alfredo di Stefano ya muda mrefu
katika Rekodi ya magoli ya Clasico baada ya kufunga bao lake kwanza tu,katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo, ambapo mchezaji huyo alipiga hat-trick katika ushindi mkubwa wa mabao 4-3 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
katika Rekodi ya magoli ya Clasico baada ya kufunga bao lake kwanza tu,katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo, ambapo mchezaji huyo alipiga hat-trick katika ushindi mkubwa wa mabao 4-3 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
![]() |
Mtandao wa GOAL.COM ulimpongeza namna hii |
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 26, alivunja Rekodi kwa kufunga bao la19,kisha tena la 20 na kuongeza lingine la 21 dhidi ya Real Madrid siku ya Jumapili katika mpambano huo wa La Liga, hivyo ni wazi amesonga mbele katika viwango vya muda wote.
Mashuhuli wa Los Blancos(Real Madrid) Di Stefano ana mabao 18 katika michezo 30 ya Clasico aliyocheza kati ya miaka 1953 na 1964, lakini Messi alimzidi kabla ya hata ya mapumziko katika mchezo wa Clasico jana jumapili , akiwa amecheza michezo 27 tu ya wapinzani hao wakubwa wa La Liga.
Messi alifungua akaunti yake ya mabao katika Clasico kwa kupiga hat-trick, katika sare ya 3-3 katika uwanja wa Camp Nou Machi 10, 2007.
Messi hajawahi kurudi nyuma ,alifunga mara mbili katika ushindi wa 6-2 kwa kuibomoa Madrid mbele ya mashabiki wao wenyewe katika uwanja wa Bernabeu Mei 2009, vilevile mshindi huyo mara nne wa Ballon d'Or pia alifunga mabao yote mawili
katika mchezo uliopigwa eneo la Blaugrana ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2 -0 na kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa 2011.
Messi aliungana na Di Stefano katika dakika ya 17 alipoifungia Barcelona bao moja katika mchezo ambao walifungwa kwa mabao 2-1katika La Liga, mchezo uliopingwa katika mji mkuu wa Hispania Machi 2
mwaka jana.
Hata
hivyo, Jumapili usiku hat-trick yake katika uwanja wa Madrid,Estadio Santiago Bernabéu , ina maana kwamba ni wazi Messi sasa imechukua milki katika Rekodi ya Clasico .
Mchezaji Lionel Messi Alfredo di Stefano Raul Gonzalez Cesar Rodriguez Francisco Gento Ferenc Puskas | klabuBarcelona Real Madrid Real Madrid Barcelona Real Madrid Real Madrid | Mabao 21 18 15 14 14 14 |
Messi,
ambaye alitoa pasi katika bao la kwanza lililofungwa Andres Iniesta usiku wa jumapili, pia amejisogeza juu ya Hugo
Sanchez kwa nafasi mbili kwenye orodha ya La Liga katika Rekodi ya wafungaji bora wa muda wote kwa mabao 236. na sasa amebakisha mabao 16 tu kumfikia Telmo Zarra anayekamata nafasi ya kwanza.
Katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo,bao la kwanza la messi lilipatikana katika dakika ya 42,na mabao mawili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 65 na 84, huku bao la kwanza la Barcelona akifunga Andrés Iniesta Luján
dakika ya 7 tu ya mchezo.
Ubabe ubabe tu:Pepe akimkaba koo Fabregas |
Wakati wakuamulia:Buesquets alimanyaga Pepe kichwani,akizuga kuwa hajamuona. |
Kwa upande wa Real Madrid ambao walikuwa nyumbani, mabao yao mawili yalimefungwa na Karim Benzema katika dakika ya 20 na 24,na bao la tatu likiwekwa nyavuni na Cristiano Ronaldo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 55.
Lakini Real Madrid walipata pigo baada ya beki wake Sergio Ramos kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 63, baada ya kumuangusha Neymar kwenye eneo la hatari.
VLakini Real Madrid walipata pigo baada ya beki wake Sergio Ramos kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 63, baada ya kumuangusha Neymar kwenye eneo la hatari.
MSIMAMO KWA SASA
Spanish La Liga |
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Atlético de Madrid | 29 | 22 | 4 | 3 | 66 | 21 | 45 | 70 |
2 | Real Madrid | 29 | 22 | 4 | 3 | 80 | 30 | 50 | 70 |
3 | Barcelona | 29 | 22 | 3 | 4 | 85 | 25 | 60 | 69 |
4 | Athletic Club | 29 | 16 | 7 | 6 | 52 | 32 | 20 | 55 |
5 | Sevilla | 29 | 13 | 8 | 8 | 53 | 44 | 9 | 47 |
6 | Real Sociedad | 28 | 13 | 7 | 8 | 49 | 39 | 10 | 46 |
7 | Villarreal | 29 | 13 | 6 | 10 | 49 | 36 | 13 | 45 |
8 | Valencia CF | 29 | 11 | 6 | 12 | 41 | 40 | 1 | 39 |
9 | Levante | 29 | 9 | 10 | 10 | 26 | 35 | -9 | 37 |
10 | Espanyol | 29 | 10 | 7 | 12 | 32 | 34 | -2 | 37 |
11 | Granada CF | 29 | 10 | 4 | 15 | 28 | 39 | -11 | 34 |
12 | Celta de Vigo | 29 | 9 | 6 | 14 | 33 | 41 | -8 | 33 |
13 | Málaga | 29 | 8 | 8 | 13 | 28 | 36 | -8 | 32 |
14 | Rayo Vallecano | 29 | 9 | 3 | 17 | 33 | 63 | -30 | 30 |
15 | Elche | 29 | 7 | 9 | 13 | 24 | 41 | -17 | 30 |
16 | Osasuna | 29 | 8 | 5 | 16 | 25 | 50 | -25 | 29 |
17 | Getafe | 29 | 7 | 7 | 15 | 26 | 46 | -20 | 28 |
18 | Real Valladolid | 29 | 5 | 12 | 12 | 31 | 49 | -18 | 27 |
19 | Almería | 28 | 7 | 5 | 16 | 27 | 52 | -25 | 26 |
20 | Real Betis | 29 | 4 | 7 | 18 | 23 | 58 | -35 | 19 |
ANGALIA VIDEO YA MABAO
Resumen Highlights Real Madrid vs FC Barcelona... by elencrrist05
Real Madrid: Diego Lopez, 7,
Pepe, 6, Ramos, 6, Cristiano Ronaldo, 7, Benzema, 8, (Varane, 64), Bale,
7, Marcelo, 7, Xabi Alonso, 7, Carvajal, 6, Modric, 7, (Morata, 90), Di
Maria, 9, (Isco, 85).
Subs not used: Casillas, Coentrao, Nacho, Illarramendi.
Scorers: Benzema, 20, 24, Ronaldo, 55 (pen).
Booked: Pepe, Di Maria, Alonso, Modric, Ronaldo.
Sent off: Ramos.
Barcelona:
Valdés, 6, Alves, 6, Piqué, 8, Mascherano, 5, Jordi Alba, 6, Busquets,
7, Xavi, 7, Iniesta, 7, Fabregas, 8, (Sanchez, 78), Messi, 10, Neymar,
7, (Pedro, 69).
Subs not used: Pinto, Bartra, Adriano Song, Sergi.
Booked: Fabregas, Busquets.
Scorers: Iniesta, 7, Messi, 42, 65 (pen), 84 (pen).
Attendance: 85,454.
Referee: Alberto Undiano Mallenco.
Man-of-the-Match: Lionel Messi
0 Comments