Ticker

6/recent/ticker-posts

ALICHOKISEMA DAVID MOYES KUHUSU ROONEY KUINGIA KATIKA HISTORIA YA MAN UNITED

 Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 24,2014 SAA 05:39 USIKU
Meneja wa Manchester United  David Moyes anaamini Wayne Rooney tayari ni mtu anayewezwa kukumbukwa katika historia ya
timu hiyo ya  Old Trafford kama Sir Bobby Charlton na Denis Law.

Rooney,tayari amefanikisha msimu wake wa  10 katika klabu hiyo,na kuwa katika orodha ya wafungaji bora wa tatu wa  United wa wakati wote kwa jumla ya mabao yake 211 na 212 katika  klabu hiyo alipo fanikisha  ushindi wa siku ya Jumamosi dhidi ya West Ham United.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa  Everton mwenye umri wa miaka 28,ambaye amewai kukosolewa katika msimu wa hivi karibuni na kuzua maswali mengi ndani ya  United , lakini yeye amebakisha mabao 26 tu kumfikia Denis Law na mabao 38 kabla ya kumfikia Charlton . 

Na Moyes anasisitiza Rooney, ambaye amerejesha nguvu baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano katika klabu hiyo, tayari ameingia katika historia ya timu hiyo. 

"Kama wewe uko katika orodha ya wafungaji bora watatu wa klabu kama Manchester United tayari ni legend," bosi huyo wa reds alisema. 

"Kama yeye hana majeraha yoyote Makubwa ana nafasi nzuri ya kuvunja Rekodi ya Denis Law na Sir Bobby Charlton kama atakuwa vizuri". 

Wapinzani wa United, Manchester City usiku wa Jumanne kama watawafunga,United wataendelea kuwa nyuma kwa alama 11 ya Arsenal walioko nafasi ya nne,huku United wakibaki katika nafasi ya saba. 

Moyes aliongeza: "Mimi sijui kama Wayne atakuwa ni mtu muhimu katika mchezo huu kwa sababu atakuwa na wachezaji wengi wa daraja la juu katika hayo mechi, lakini yeye nina uhakika ni mmoja wao." 

Post a Comment

0 Comments