Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:MICHUANO YA NETBALI YA KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI, YAANZA LEO UWANJA WA TAIFA

Na.Herman kihwili,IMEWEKWA March. 22,2014 SAA 03:48 USIKU
Michuano ya Netiboli ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki kwa wanawake na wanaume imeanza kutimua vumbi hii leo katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa JKU Zanzibar akifunga goli
Michuano hiyo inayohusisha timu takrbani 18 kutoka katika ukanda huu,imeanza leo kwa kupingwa michezo miwili.Ambapo mchezo wa ufunguzi ulikuwa ni kati ya Timu ya kutoka Uganda na Magereza ya Tanzania,na katika mchezo huo timu ya Uganda imechomoka na ushindi wa magoli 55 dhidi ya magoli 21 ya Magereza ya Tanzania.
Mabingwa watetezi kwa mwaka jana wa michuanao hiyo kwa wanaume ambao ni Magereza Kenya (kijani) wakipambana na washindi wa pili wa michuanao hiyo mwaka jana. JKU Zanzibar (nyekundu)
Mchezo wa pili ulikuwa ni kati ya JKU ya Zanzibar na timu Magereza ya Kenya,na katika mchezo huo timu ya Magereza ya Kenya imechomoka na ushindi wa magoli 43 dhidi ya magoli 32 ya timu ya JKU.
Kocha wa JKU Zanzibar akitoa maelekezo
Mchezo ulimalizika kwa Timu ya Magereza Kenya kuibuka na ushindi wa magoli 43 dhidi ya magoli 32 ya timu ya JKU Zanzibar
wachezaji wa timu ya Magereza Kenya wakipongezana baada ya ushindi
Wachezaji wa Timu ya JKU Zanzibar ambao ni washindi wa pili wa mwaka jana kwa wanaume wakijilaumu wenyewe baada ya mchezo kumalizikia
Michuano hiyo itaendelea tena kesho siku ya jumapili saa 3 asubuhi kwa timu mbalimbali kupambana katika uwanja wa Taifa,ni bure hakuna kiingilio.

Post a Comment

0 Comments