Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 21,2014 SAA 02:22 USIKU
Mfungaji bora wa Manchester City Sergio Aguero atakosa derby ya wiki ijayo
dhidi ya Manchester United kutokana na kuwa
majeruhi, meneja Manuel
Pellegrini amethibitisha leo siku ya Ijumaa.
Aguero anaendelea kuuguza majeraha ambayo aliyapata wakati timu yake ikicheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao walifungwa na
Barcelona wiki iliyopita na Pellegrini anasema kwamba "hakuna
nafasi" kwa mchezaji huyo kuanza safari ya Old Trafford siku ya Jumanne.
Aguero, ambaye alifunga mabao 26 msimu huu, anaweza kurudi katika mchezo dhidi ya Arsenal siku ya tarehe 29 March.
"Sisi bado hatujui, lakini labda wiki ijayo ataanza kufanya kazi na kikosi," Pellegrini alisema.
"Sidhani kama ni wiki nzima. Labda mwishoni mwa wiki anaweza kuwa na kikosi na kuanza mazoezi."
Alipoulizwa kama nyota huyo wa kimataifa wa Argentina atakuwa katika mpambano watakaokutana na United, Pellegrini alijibu: "Kwa United,hapana,hana nafasi."
Akizungumza
kabla ya timu yake ambayo itakuwa nyumbani ikipambana na Fulham siku ya Jumamosi,
Pellegrini pia aliongeza kwa kukanusha uvumi kuwa Aguero yuko katika harakati za uhamisho kwenda Barcelona.
"Hatuwezi
kuzungumza kila wiki kuhusu wachezaji ambao wako hapa Manchester
City na wachezaji kuwa wata kwenda nje. Yeye ni mchezaji wa Manchester
City, yeye anafuraha sana hapa katika klabu na tuna furaha sana pamoja naye pia."

0 Comments