IMEWEKWA March. 21,2014 SAA 01:32 USIKU
Yanga inaumana na Rhino Rangers katika moja kati ya
mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa
wikiendi hii katika
miji miwili tofauti.
Mechi hiyo itafanyika kesho (Machi 22 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora ambapo kiingilio kitakuwa sh. 5,000
kwa jukwaa kuu na sh. 3,000 mzunguko.
Nayo JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika
mechi itakayochezwa kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam
kuanzia saa 10 kamili jioni.
Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Jumapili) kwa
mechi nne ambapo Simba itacheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Azam itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Mechi hizo mbili zitakuwa ‘live’ kupitia Azam Tv.
Mechi nyingine za Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi
ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting
na Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani
Pwani.
0 Comments