Ticker

6/recent/ticker-posts

HII NDIO SHEREHE ATAKAYOIKOSA KIM POUSIN

IMEWEKWA FEB. 28,2014 SAA 10:32 JIONI
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Kim Pousin na Rais wa Tff Jamali Malinzi wakipeana mkono mara baada ya mkutano na waandishi habari siku ya jana baada ya kusitisha mkataba wake, kocha huyo atakosa maadhimisho ya miaka 50 ya TFF ya kujiunga na FIFA akiwa kama kocha wa Taifa Stars.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho
ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.

Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).

Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi karibuni.

Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.

Post a Comment

0 Comments