Ticker

6/recent/ticker-posts

TFF YAWATAKA MADAKTARI VPL KUWASILISHA VYETI,PAMOJA NA KUPIGA MARUFUKU WACHEZAJI WASIOPIMA AFYA ZAO

Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA JANUARI 28,2014 SAA 09:07 MCHANA
Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu
wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8 mwaka huu.

Wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa wachezaji.

Pia TFF itatoa kwa madaktari hao fomu maalumu za vipimo kwa wachezaji ambapo kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vyote kama ambavyo fomu imeelekeza.

Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya wachezaji.

Post a Comment

0 Comments