IMEWEKWA JANUARI 28,2014 SAA 08:27 USIKU
![]() |
| Athuman Idd |
Kiungo wa ulinzi wa timu ya Young Africans Athuman Idd Athuman
"Chuji" amerejeshwa kundini kuungana na wachezaji
wenzake baada ya awali
kuwa amesimamishwa na uongozi kutona na kitendo cha utovu wa nidhamu
aliouonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
Athuman Idd "Chuji" alisimamishwa na uongozi na Young Africans baada
ya kuonyesha utovu wa nidhamu na kuamua kuondoka vyumbani kuelekea
nyumbani kabla ya mchezo kumalizika kitu ambacho alikiri ni makosa mbele
ya uongozi.
Uongozi wa Young Africans ulifikia kumpa barua ya
kumsimamisha Chuji ambaye alikiri kufanya kosa hilo na kisha kukiri
mbele na kuandika barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutorudia tena
kitendo hicho au kufanya kitendo kingine chochote cha utovu wa nidhamu.
Baada
ya kuandika barua kwa uongozi kuomba msamaha, Chuji alipewa onyo kali
na uongozi na kupewa kipindi cha matazamio ambapo kwa kipindi cha mwezi
mmoja ameonekana kubadilika na kurejea katika nidhamu ya hali ya juu
ndani na nje ya uwanja.
Chuji
ataungana na kikosi cha Young Africans kesho tayari kwa mikikimikiki ya
Ligi Kuu pamoja na mashindinao ya Klabu Bingwa Afrika ambayo
yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo kwa Young Africans kuanza na
timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro.
CHANZO: www.youngafricans.co.tz
CHANZO: www.youngafricans.co.tz

0 Comments