Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 28,2014 SAA 09:58 ALFAJIRI
Rais mpya wa Barcelona
Josep Maria Bartomeu amesisitiza Lionel Messi hauzwi na anasema klabu hiyo nia ya kuanza mazungumzo juu
ya mkataba mpya
na nyota huyo wa Argentina hivi karibuni.
Messi
aliongeza mkataba wa miaka miwili na Barca mwezi
Februari uliopita, ambapo mkataba wake na klabu unafika tamati hadi Juni 30, 2018, lakini
mabingwa hao wa Kihispania wako tayari kujadili mkataba mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Bartomeu,
ambaye alichukua majukumu ya urais wa klabu ya Barca siku ya Alhamisi usiku kufuatia Sandro Rosell kujiuzulu ghafla , pia alionya hali ya uwezekano kwamba Messi hayuko katika soko, huku kukiwa na taarifa za mchezaji huyo kuzivutia klabu kubwa ikiwemo ya mabingwa wa kutumia wa Kifaransa, Paris Saint-Germain.
Akizungumza na kituo cha redio cha Kikatalani, RAC1, Bartomeu alisema: "Messi si kwa ajili ya kuuzwa".
"Tunataka
kukaa chini bila kurukaruka, na baba yake pamoja na wakala wake kwa
sababu tunataka kuhakikisha kuwa yeye ni mchezaji bora ambaye analipwa kama anavyostahili."
Messi
alifikisha mechi 400 akiwa na Barca wiki iliyopita katika
robo-fainali ya kwanza ya Copa del Rey dhidi ya Levante na amefunga magoli 331
hadi sasa kwa klabu hiyo kubwa ya Kikatalani.
Katika
wakati wake akiwa Nou Camp, Messi alishinda Ballon d'Or rekodi mara nne, na vile
vile kusaidia Barca kushinda vikombe kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ligi kuu ya Spain mara sita, Ligi ya Mabingwa mara tatu na Copa del Rey mara mbili.

0 Comments