Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 28,2014 SAA 07:45 USIKU
Gareth Bale
atakosa mechi ya Kombe la Mfalme ya robo fainali ya pili siku ya Jumanne watakapokuwa nyumbani wakipambana na timu ya
Espanyol kutokana na tatizo la kuumia kwa mguu wake wa kushoto, kocha Carlo
Ancelotti alisema siku ya Jumatatu.
Bale
ambaye alianza katika mechi tatu zilizopita za Madrid, alibadilishwa katika kipindi cha pili siku ya Jumamosi kabla ya kuanza kusikia maaumivu mapema tu katika kipindi cha kwanza walipoibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Granada katika uwanja wa
Bernabeu.
| Kujeruhiwa: Gareth Bale atakosa mechi ya Copa del Rey ya robo fainali ya pili kutokana na kuumia mguu wakati Real Madrid watakapopamba na Espanyol |
| Ouch: Bale aliumia katika maungiao ya mguu wake ,katika mchezo ambao walishinda mabao 2-0 dhidi Granada katika uwanja wa Bernabeu siku ya Jumamosi |
Nyota huyo wa kimataifa,ameharibiwa msimu wake kutokana na majeraha madogo madogo tangu
uhamisho wake ambao uliweka rekodi akitokea katika klabu ya Tottenham Hotspur mwaka jana.
Ancelotti alisema hawezi kutoa mafunzo kwa mchezaji huyo aliye mapumziko siku ya Jumatatu.
"Yeye hana tatizo na sehemu zake za siri,zinalipa vizuri , (akitania kwa lugha ya Italia),Lakini hayuko vizuri na mguu wake wa kushoto utaathiri usawa wake kidogo."
"Alijaribu
kufanya mazoezi lakini yeye hayuko vizuri na tunaepuka kuuweka mchezo wa jumapili katika hatari,na ndio maana nikampumzisha ," alisema Ancelotti
akimaanisha ratiba ya ligi kuu na kuwa nafasi ya nne chini ya Athletic Bilbao.
| Nifuateni mimi, Cristiano Ronaldo na Luka Modric (mbele) wakifanya mazoezi |
Real wanafaida ya goli 1-0 zaidi ya Espanyol kutokana na mechi ya kwanza iliyopingwa katika uwanja wa Estadi Cornella-El Prat
0 Comments