Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 28,2014 SAA 07:45 USIKU
Cardiff
City wamemsaini mchezaji wa Manchester United ambaye ni raia wa Brazil Fabio na mshambuliaji wa Stoke
City Kenwyne
Jones, meneja wa klabu hiyo ya Ligi Kuu Ole
Gunnar Solskjaer alisema siku ya Jumatatu.
Cardiff
pia wana matumaini ya kumuajiri winga wa Manchester United Wilfried Zaha kwa
mkopo kabla ya mwisho wa dirisha dogo la uhamisho siku ya Ijumaa.
"Fabio
na Kenwyne wataungana na katika mazoezi siku ya leo,nimekutana nao na kwamba na hii ni zaidi ya kile tunachokifanya," Solskjaer
aliwaambia waandishi wa habari huko Manchester kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya United siku ya Jumanne.
Solskjaer ambaye ni raia wa Norway , ambaye pia amechukua majukumu ya kuinoa Cardiff mwezi huu, alisema mpango wa Zaha ilikuwa bado haujakamilika.
"Tunatumaini kufanikisha jambo hilo katika masaa 24 yajayo au hivyo, ili aweze kuwa
tayari kwa ajili ya mwishoni mwa wiki,"mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United
alisema.
Cardiff katika msimamo ipo katika nafasi ya chini kabisa na iko katika hatari ya kushushwa daraja kufuatia kupanda daraja katika Ligi Kuu kwa mara ya kwanza mwaka jana.

0 Comments