Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA JANUARI 31,2014 SAA 11:57JIONI
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaingia raundi ya 16 wikiendi
hii kwa mechi nne ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa
Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Refa atakuwa Nathan Lazaro kutoka mkoani
Kilimanjaro wakati Kamishna ni Hakim Byemba wa Dodoma.
Uwanja
wa Azam uliopo Mbagala siku hiyo kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Ashanti
United na Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga kwa viingilio vya sh. 3,000
kwa sh. 10,000.
Jumapili
(Februari 2 mwaka huu) ni Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
saa 10 kamili jioni), na Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
saa 10 kamili jioni).
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania
Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu
Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi).
BODI YA LIGI
YAZIPIGA JEKI KLABU ZA FDL
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL).
Uamuzi
wa kuzisaidia timu hizo ulifanywa katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye
akaunti za klabu husika. Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB
zinatakiwa kuwasilisha haraka.
Klabu
za FDL ni African Lyon, Burkina Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa
JKT, Kimondo, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na
Mwadui.
Nyingine
ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro,
Polisi Tabora, Stand United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.

0 Comments