Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 31,2014 SAA 10:58 JIONI
Klabu ya Chelsea leo hii Ijumaa imemsaini Kurt Zouma kutoka St.
Etienne.na mchezaji huyo atabaki kwa mkopo katika klabu hiyo ya
nchini Ufaransa mpaka mapumziko ya msimu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ni mlinzi wa kati na amejiunga na klabu ya Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano na nusu,na amejiunga kwa ada inayoaminika kuwa £ 12.5m.
Zouma ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21,amezaliwa mjini Lyon na kujiunga na St. Etienne akiwa na umri wa miaka 15.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema Zouma ni mchezaji wa nne kusainiwa na Chelsea katika dirisha hili la uhamisho,kufuatia kumchukuwa kiungo Nemanja Matic kutoka Benfica, Mohamed Salah kutoka
Basel na Bertrand Traoré, ambaye mara moja alipelekwa kwa mkopokatika timu ya Vitesse Arnhem.

0 Comments