Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 31,2014 SAA 09:08 USIKU
Liverpool
na Tottenham inaeleweka wanagombania saini ya winga wa Dnipro
Dnipropetrovsk, Yevhen Konoplyanka kabla ya tarehe ya
mwisho wa dirisha dogo la uhamisho siku ya Ijumaa usiku.Mkurugenzi mtendaji wa Liverpool Ian Ayre amekwenda nchini Ukraine wiki hii kujadili juu ya kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 , ambaye amecheza mechi 35 kwa ajili ya nchi yake.
Hata
hivyo, imebainika kuwa Livepool wanakumbana na ushindani kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya
sahihi ya mchezaji huyo, ingawa inaeleweka kuwa timu kutoka Anfield ndio wamebaki katika nafasi ya kumnyakuwa mchezaji huyo.
Liverpool
bado hawaja sajili mtu yeyote mwezi huu na walimkosa winga kutoka Misri Mohamed Salah,
ambaye aliondoka katika klabu ya Basel na kutua Chelsea licha ya kufanya mazungumzo kuhusu kuhamia Anfield.
Kufuatia
ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Everton katika Ligi Kuu siku ya
Jumanne, meneja Brendan Rodgers alisema kuwa yeye alikuwa na matumaini " makubwa ya kumsaini mchezaji huyo".
"Nadhani sisi tunamatumaini kufanya kitu siku chache zijazo," alisema.
Mipango
wa Rodgers bado unaweza kushindikana tena, kama viongozi wa Tottenham watasimamia na kukubaliana uhamisho huo wa Konoplyanka kabla ya dirisha kufungwa
siku ya Ijumaa usiku.
Konoplyanka,
ambaye alifunga dhidi ya Uingereza mchi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014
katika uwanja wa Wembley Septemba 2012,anaweza kucheza upande wowote.
Baba wa mchezaji huyo Oleg aliongelea kuhusiana na tetesi za uhamisho wa mchezaji huyo kutua Anfield na kuwaambia
vyombo vya habari vya Kiukreni kuwa: "Sitaki kusema hasa lakini
taarifa kuhusu uhamisho wa klabu za Uiingereza ni kweli".
"Yeye anaweza kubadili klabu baadaye wiki hii. Hatuzingatii ofa kutoka Ukraine" alisema baba wa mchezaji huyo.

0 Comments