Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 31,2014 SAA 02:58 JIONI
Mkali wa kuzifumania nyavu kutoka Manchester
City Sergio Aguero anatarajiwa kuwa nje kwa mwezi kutokana na kuumia misuli katika mguu, Meneja wa klabu hiyo Manuel Pellegrini alisema siku ya Ijumaa.
Mshambuliaji
wa huyo wa Argentina aliumia misuli yake baada ya
kufunga bao katika mchezo ambao walishinda 5-1 dhidi ya Tottenham Hotspur siku ya Jumatano ambapo uliwafanya City kuwa juu katika msimamo wa Ligi Kuu,lilikuwa ni goli lake la 26 la msimu katika mechi 22 tu.
Atakosa michezo muhimu yote dhidi ya Chelsea katika Ligi Kuu na
Kombe la FA na mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona.
"Sergio ni mchezaji wa kwetu lakini nadhani tunaweza kuchukua nafasi yake," Pellegrini aliwaambia waandishi wa habari. "washambuliaji wengine wote , Alvaro Negredo, Edin Dzeko na Stefan Jovetic watachukua nafasi yake"

0 Comments