IMEWEKWA JANUARI 10.2014 SAA 04:37 USIKU
Meneja wa Manchester United David Moyes imeshtakiwa kwa utovu wa nidhamu na Chama cha Soka FA kwa maoni yake
katika mechi dhidi ya Sunderland katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la Ligi ambapo walifungwa mabao 2 kwa 1 siku ya Jumanne.
Bosi huyo wa Manchester United alimkosoa mwamuzi Andre Marriner pamoja na wasaidizi wake kutokana na kipigo hiko.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 50 alisema kuwa timu yake inacheza dhidi ya waamuzi pamoja na timu pinzani.
“Sote tulikuwa tukiwacheka (marefa) wakati huo. Inaonekana ni kana
kwamba tunacheza dhidi yao (marefa) pamoja na wapinzani kwa sasa.”alisema
Katika taarifa
ambayo ilitolewa kwa tahadhari na FA, ambayo wanadai Moyes "ameshtakiwa kwa kosa linaloitwa uadilifu wa mwamuzi katika mechi, / na alisema kuwa
viongozi wale katika mechi walikuwa na motisha kwa upendeleo; / au na kuleta mchezo kwa jina baya."
Moyes ameambiwa hadi siku ya tarehe 15 Januari saa 6:00 mchana awe amejibu mashtaka ya FA, na anatarajiwa kukutana na faini kama atapatikana na hatia.
0 Comments