IMEWEKWA DESEMBA 7.2013 SAA 10:44 ALASIRI
Nahodha wa kikosi cha Young Africans U20 - Issa Ngao |
Nahodha wa kikosi cha Young Africans U-20 ambaye pia msimu huu
amepandishwa katika kikosi cha kwanza Issa Rashid Ngao
amesema
ameshangwaza na taarifa zilizotolewa jana katika baadhi ya mitandao
kwamba yeye hana mkataba na Yanga na kusema hizo ni taarifa za uongo.
Ngao ambaye katika mashindano ya Uhai Cup yaliyomalizika mwishoni mwa
wiki aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo amesema anashangazwa na
taarifa hizo ambazo hazina ukweli wowote na kwamba yeye ni mchezaji wa
Yanga kwa mkataba ndio maana analipwa haki zake kila mwisho wa mwezi.
Kiukweli
hata mie nashangaa, sijui habari hizi hata wamezitoa wapi, hawajaongea
na mimi kuweza kupata ukweli lakini cha ajabu hata hawakuweza kuwauliza
viongozi wangu.
"Mimi ni
mchezaji wa U20 Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili, nilisajiliwa
siku moja pamoja na wachezaji wenzangu Rehani Kibingu, George Banda,
Yusuph Abdul, Notikely Masasi na Mwinyi Bakari na wegine wengi
tu"alisema Ngao
Aidha Afisa Habari wa klabu ya Young
Africans Baraka Kizuguto amesema ameshangwazwa na taarifa hizo ambazo
hazijafanyiwa upembuzi akinifu kabla ya kutolewa kwa jamii, ukweli ni
kwamba wachezaji wote Yanga wana mikataba na wanalipwa haki zao kila
mwezi.
Hakuna mchezaji anayecheza bure Yanga wala bila kuwa na
mktaba na kama kuna wanaojidanganya hivyo basi imekula kwao, vijana wote
wa timu ya U20 wanatambulika na viongozi kwa ngazi zote kutokana na
kutambulika kwa ajira zao ndani ya Yanga.
Issa Rashid Ngao pamoja
na kuwa ni mchezaji wa timu zote za Yanga ya wakubwa na vijana U20, pia
anaendelea na masomo katika chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es salaam
akisomea Bachelor of Arts in Education (BAE) akiwa mwaka wa pili sasa.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz
0 Comments