Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 7.2013 SAA 07:44 USIKU
Mtangazaji wa BBC Huw Edwards ametoa machozi wakati alipokuwa akitangaza taarifa za mapema kabisa (BREAKING NEWS) kuhusiana na
kifo cha Nelson Mandela.
Sauti ya mtangazaji huyo mzoefu ilikuwa na mawimbi wakati akiwa
anatangaza matangazo ya moja kwa moja(LIVE) ndani ya BBC News
baada ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kutangaza kifo cha Mr Mandela. Mr Edwards alionekana na uso wa huzuni baada ya kutangaza habari za kifo cha Mr Mandela ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuungua kwa muda mrefu kwa sababu ya matatizo ya mapafu.
Watu katika mtandao wa kijamii wa Twitter,walitoa maoni ya kumpongeza Mr Edwards kwa "kipaji"
kwani alikuwa akifanya kazi licha ya kuangalia kama yeye alikuwa "anaumia ndani na kutoa machozi".
Mtumiaji mmoja wa Twitter anaitwa Geraint Lloyd aliandika: "Huw Edwards unafanya kazi ngumu usiku
wa leo,licha kwa kiasi gani ni wazi unamaanisha unachokifanya."
Mwingine anayeitwa Glyn Morgan aliongeza: "Huw Edwards ni wazi umenigusa #
bbcnews channel,wote tunatokwa na machozi."
Na
Nicola Bitton pia aliandika: "matangazo ni mazuri,kwa kiasi kikubwa yamebebwa
na muonekano wa kusikitishwa wa Huw Edwards ndani ya BBC News usiku wa leo, kwa dhati atasonga sana."
Mtandao wa kijamii wa Twitter ulitawaliwa na maombolezo ya Mr Mandela, kwa kutawaliwa na #RIPNelsonMandela zilizovuma juu ya mitandao huo wa kijamii .
Watu maarufu na wanamichezo kutoka duniani kote walitumia Twitter na mitandao mingine kama Facebook kutoa rambirambi zao baada ya kifo cha Mr Mandela.
Na blog ya Jamii na Michezo inasema RIP Nelson Mandela.
0 Comments