Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 19.2013 SAA 12:00 ASUBUHI
O oo!Utata: Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere alionekana kufanya ishara hii kuelekeza mashambulizi kwa mashabiki wa City |
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere amekubali mashtaka kutoka Chama cha Soka cha FA kwa madai yaliyotolewa siku ya Jumamosi baada ya kuwaonyesha mashabiki wa Man City ishara ya kidole cha kati,lakini lazima atagomea adhabu ya kupingwa marufuku mechi mbili,BBC wametoa taarifa hiyo siku ya Jumatano.
Ishara hiyo inayochukuliwa kama ni matusi,na aliionyesha sekunde chache baada ya mchezo kumalizika ambao Arsenal ilifungwa 6-3 .
Tukio
hilo lilitokea katika uwanja wa Etihad Desemba 14,halikuonekana na mwamuzi Martin Atkinson na maofisa wa mechi lakini lilionekana kupitia katika video.
Wilshere alijitahadi kuhisaidia Arsenal lakini walipotea katika uwanja wa Etihad |
Wilshere alishtakiwa kujibu mashtaka hayo ya chama cha FA, chini ya mradi mpya wa
majaribio unaojulikana kama 'kuto kuonekana' matukio katika mechi za Ligi Kuu.
Kufuatia
kushtakiwa huko na FA jopo la wanachama wote watatu walikubaliana kwa kauli moja kutoa adhabu.
Siku mbaya katika ofisi: Wilshere akivua shati lake baada ya timu yake kufungwa 6-3 katika uwanja wa Man City |
Kesi
yake itasikilizwa na tume siku ya leo Alhamisi na kama atasimamishwa ataweza kukoa mechi ya ligi kuu kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea tarehe 23
Desemba na mchezo wa West Ham United siku tatu baadaye.
0 Comments