Ticker

6/recent/ticker-posts

HII NDIYO SABABU YA MMILIKI WA TIMU YA HALL CITY KUTAKA KUBADILI JINA LA KLABU HIYO

IMEWEKWA DESEMBA 12.2013 SAA 02:41 USIKU
Klabu ya Ligi kuu nchini England Hull City imewasilisha ombi kwa FA ya Uingereza kutaka kubadilisha jina lake la Hull City  na
kuitwa Hull Tigers kuanzia msimu ujao. 


Mmiliki wa klabu hiyo Assem Allam anataka kubadilisha jina klabu hiyo yanye umri wa miaka 109 kutoka Yorkshire lakini hatua hiyo imepingwa vikali na mashabiki wa klabu hiyo. 

Mfanyabiashara huyo mzaliwa wa Misri tayari alibadilisha jina la kampuni inayomiliki klabu hiyo kutoka Hull City Association Football Club hadi Hull City Tigers mwezi Agosti. 

Allam anaamini kwamba nembo ya 'Tigers' “itauza zaidi ulimwenguni”. 

Mashabiki sugu wa Hull wameapa kupinga hatua zozote za kubadilisha jina la klabu hiyo na wameunga kundi kwa jina "City Till We Die" (City Hadi Kufa Kwetu).

Post a Comment

0 Comments