IMEWEKWA NOVEMBA 10.2013 SAA 01:02 USIKU
Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Young
Africans umesema hauna mpango wa mazungumzo yoyote
na aliyekua kocha
mkuu wa timu ya Azam FC muingereza Stewart Hall juu ya kumpa ajira ya
kuwa kocha na Ernie Brandts bado anaendelea na kazi yake ya ukocha mkuu.
Taarifa hii ya uongozi wa klabu ya Yanga inafuatia kuzagaa kwa
taarifa hizo leo mchana kwenye baadhi ya mitandao mbali mbali ya kijamii
kuwa wapo katika maongoezi na kocha huyo ili achukue nafasi ya kocha
mholanzi Ernie Brandts.
Msiumizwe vichwa na taarifa hizo kwani
wengi wao lengo lao ni kutaka kuivuruga Yanga sasa ili isiweze kufanya
vizuri katika mzunguko unaofuata na mashindano ya kimataifa, uzuri
tumelijua hilo na sisi tunauambia umma hatuna mazungumzo na kocha huyo
na wala hatujawahi fikiria kufanya hivyo.
Tunaomba
umma wa wapenzi wa soka nchini, wanachama, washabiki na wapenzi wa
Young Africans watamabue kuwa Ernie Brandts bado ni kocha mkuu wa klabu
yetu na hatuna mpango wa kufanya mabadiliko na wala hatujawahi kufikiria
kufanya hivyo.
Mholanzi
Ernie Brandts anatarajiwa kurejea nchini jumapili Novemba 24, 2013
tayari kabisa kwa kuanza mazoezi na vijana wake siku ya jumatatu Novemba
25, 2013 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Hisani (Nani Mtani Jembe)
dhidi ya Simba SC Disemba 14, 2013.
Mara
baada ya mchezo huo kikosi kitaendelea na maandalizi kujiandaa na
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na mashindano ya kimataifa lakini
pia timu inategema kushiriki wa mashidano ya Mapinduzi Cup kisiwani
Zanzibar mapema mwezi Januari 2014.
Msimu wake wa kwanza
ameiongoza Yanga kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na hivi sasa
anaongoza msimamo wa Ligi kwa kuwa na pointi 28 na mabao 31 ya kufunga
na mabao 11 ya kufungwa.
Kocha Brandts mara baada ya mchezo wa
mwisho dhidi ya JKT Oljoro alitoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji
wake na benchi la ufundi kwa ajili ya kuwa na familia zao na mapumziko
na ambapo timu inatarajiwa kuanza tena mazoezi tarehe 25 Novemba
kujiandaa na michezo itakayokuwa inawaikabili timu.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz

0 Comments