Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 11.2013 SAA 10:04 JIONI
Klabu ya Barcelona imethibitisha kwamba Lionel Messi atakuwa nje tena kwa zaidi ya majuma 6 hadi 8 baada ya kuumia mguu
katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya timu ya Real Betis siku ya jumapili.
katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya timu ya Real Betis siku ya jumapili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliumia mguu wake wakati akijaribu kuongeza kasi wakati akiwa na mpira miguuni mwake katika dakika ya 18 tu ya mchezo.
Messi ambaye ameumia katika mguu wake wa kushoto,atakuwa akifanyiwa vipimo zaidi siku ya Jumatatu,na kocha wa Barca Gerardo Martino amesema"Sijui lolote kuhusu dawa ila nami nasubiri kuona nini madaktari wanasema kuhusu ukubwa wa kuumia kwake".
"Tunahitaji pia kuzungumza na Leo, ni vipindi vitatu na amekuwa katika muda mfupi hivyo ni wazi atacheza akiwa na mawazo juu yake."
Mchezaji huyo wa Kimataifa
wa Argentina na mchezaji wa mwaka wa Dunia, pia alikuwa nje mwezi Agosti
baada ya mechi dhidi ya Atletico Madrid kwa matatizo ya ukano wa mvungu wa goti,na alijeruhiwa mguu katika mechi dhidi ya Almeria mwezi September.
"Kamwe si habari njema ikiwa mchezaji anaumia tena kwa mara nyingine, na juu ya yote
wakati yeye jina lake la Lionel Messi ni mmoja wa walioitwaye,Maoni yangu ni kwamba hatuwezi kukimbilia kumrudisha," aliongeza mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Andoni Zubizarreta.

0 Comments