MEWEKWA NOVEMBA 9.2013 SAA 12:09 JIONI
![]() |
| Juma Kaseja akisani mkataba wa kuicheza Yanga kwa miaka miwili mbele ya mwenyekiti wa kamati ya mashindano Bin Klebl |
Mlinda mlango nambari moja nchini Tanzania kwa kipindi kisichopungua
miaka 10 mfululizo Juma Kaseja Juma jana majira ya
saa 2 usiku alisaini
mkataba wa kuitumikia klabu ya Young Africans yenye makao yake
Twiga/Jangwani kwa kipindi cha miaka miwili.
Usajili wa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya Yanga unafuatia
mapendekezo ya benchi la ufundi katika ripoti waliyoikabidhi kwa kamati
ya mashindano kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa ajili mzunguko wa pili
na mashindano ya kimataifa.
Benchi la ufundi chini ya kocha mkuu
Ernie Brandts lilihitaji mlinda mlango mwenye uzoefu wa michezo ya
kimataifa kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kimataifa na mzunguko wa
pili ambao utakua na upinzani kulingana na kila timu kutaka kufanya
vizuri.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara
baada ya kumalizika kwa zoezi hilo mwenyekiti wa kamati ya usajili wa
klabu ya Yanga Abdallah BinKleb alisema hawana shaka na uwezo wa Kaseja
kwani rekodi yake ndani na nje ya nchi inafahamika kwa hiyo wanaamini
atatoa mchango mkubwa wa timu ya Yanga.
Timu yetu
imekamilika kila idara, kikubwa tunachokifanya ni kuhakikisha tunazidi
kukiboresha na kuyafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi ili
kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri na kutisha katika Ligi Kuu
ya Vodacom na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
"Najua wegine
watajiuliza maswali mengi kwa nini Yanga wamemsajili Kaseja, ukweli ni
kwamba walinda mlango waliopo ndani ya Tanzania Kaseja bado ana uwezo
nkubwa na msaada ambao atautoa katika kukiimarisha kikosi chetu" alisema
Bin Kleb
Kaseja hakua na timu yoyote aliyoichezea katika mzunguko
wa kwanza wa Ligi Kuu kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na timu yake
ya zamani ya Simba SC hivyo kujiunga na Yanga kama mchezaji huru katika
kipindi hichi cha drisha dogo la usajili.
Kutua kwa Kaseja
kunaifanya Yanga kuwa na walinda mlango wanne wote wenye uwezo wa hali
ya juu na kutokuwa na shaka wakati wowote timu inapokuwa inakabaliana na
mashindao yoyote iwe ni ndani ya nchi au ya nje ya nchi (kimataifa).
Kaseja
anaungana na walinda mlango wengine Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius
Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul ambao wataitumikia klabu ya Yanga
kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom januari 2014 na
mashindano ya klabu Bingwa Afika 2014.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz

0 Comments