Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 9.2013 SAA 12:09 JIONI
Ronaldinho ambaye aliumia mguu, ameongezeka wepesi kuliko ilivyotarajiwa na klabu
yake ya Atletico Mineiro na sasa wanasema
anauwezekano wa kucheza
katika mashindano ya klabu ya Kombe la Dunia nchini Morocco mwezi Desemba.Kiungo huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa katika mazoezi siku ya Ijumaa na kocha CUCA aliwaambia waandishi kuwa angeweza kurudi katika mchezo dhidi ya Fluminense katika Serie A ya Brazil Desemba 1.
"Tuna
matumaini ya kumtumia kabla ya msimu wa ligi kumalizika, labda
mwisho au ya pili kutoka mechi ya mwisho, hatuna tarehe kamili lakini nguvu zake zimerudi tena na anaendelea vizuri sana "" alisema CUCA katika mkutano na waandishi habari.
Ronaldinho alipata matatizo baada ya kuraruliwa misuli katika mguu wake wa kushoto mwezi Septemba na walikuwa
wanaogopa huenda angekosa mashindano ya Afrika ya Kaskazini.
Atletico
Mineiro watakutana na wapinzani ambao bado hawajajulikana katika nusu fainali ya
Desemba 18 na wanatarajia kukutana na washindi wa Ligi ya Mabingwa
Bayern Munich katika fainali siku tatu baadaye.

0 Comments