Ticker

6/recent/ticker-posts

AZAM FC YATANGAZA SIFA ZA MRITHI WA STEWART HALL,LAKINI WASEMA MILANGO IKO WAZI KAMA KOCHA WA YANGA AKIPELEKA MAOMBI



 Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 11.2013 SAA 03:30 USIKU

Uongozi wa timu ya Azam Fc ya jijini Dar es saalam,umesema mchakato wa kumpata kocha mpya klabu hiyo bado unaendelea,na
kamati iliyokabiziwa jukumu la kumtafuta kocha,inaendelea kufanya kazi yake ,ili kuweza kumpata kocha atakayeweza kulimudu soka la Afrika.
Akizungumza na Jamii na Michezo msemaji wa Azam Fc  Jaffari Idd amesema,klabu hiyo inamtafuta kocha mwenye vigezo,atakayeweza kuichukuwa timu kutoka pale Stewart Hall alipoacha na kuweza kuwaendeleza,kwa maana bado wanachangamoto nyingi ikiwemo ligi kuu katika awamu ya pili na mashindano ya kimataifa.
“Ili tuweze kufanya vizuri tunaitaji kupata kocha ambaye ana uwezo na ambaye anaweza maisha ya Afrika na kujua kwamba wachezaji wakiafrika wako vipi,kwa mfano unamchukua kocha wakati mwingine kutoka Italy huko,ujui kitu chochote  ambacho kinafanyika hapa Afrika, ajua tabia za wachezaji wa Afrika.kwahiyo lazima upate kocha ambaye amewai kupata nafasi ya kuweza kufundisha soka katika nchi yeyote ya kiafrika”alisema Jaffari Idd.

Aidha Jafari iddi ameongeza kuwa kwa sasa zoezi la kumtafuta kocha ambaye anawafaa bado linashungulikiwa,na endapo litakamilika watatoa taarifa za kocha yupi ambaye wamempitisha au nani ambaye ametoa maombi ya kuitaji,ila kwa sasa lazima wapate muda kwa kuwa swala la kumtafuta kocha sio swala dogo,kwani ukikosea katika swala la kumpata kocha mzuri basi mfumo wote utakuwa umeharibika.
Pia amekana taarifa zilizoenea jijini kuwa Azam fc inamtaka kocha wa timu ya Yanga Ernie Brants  na kusema wala hawajapata maombi yeyote kutoka kwa kocha huyo,na wala Azam fc haijamfuata kocha huyo na kumwambia kama inamuitaji,lakini kama akituma maomgi ya kutaka kazi ya ukocha katika klabu ya Azam Fc,ataangaliwa sifa zake kama anafaa au hafai.

Post a Comment

0 Comments