Na.Ezekiel Kamwaga.IMEWEKWA AGOSTI 25,2013 SAA 10:00 jioni
MWENYEKITI wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, leo mchana
amefanikisha upatikanaji wa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa
wachezaji wawili wa klabu hiyo kutoka nchini Burundi -Amissi Tambwe na
Gilbert Kaze.
Wachezaji hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya
taifa ya Burundi (Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi
Kuu ya Tanzania iliyochezwa jana kutokana na
kutokamlika kwa uhamisho huo, jambo lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji wenyewe, uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu.
kutokamlika kwa uhamisho huo, jambo lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji wenyewe, uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu.
Rage
aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku na imechukua chini ya saa 24
kuweka kufanikisha suala hilo. Katika taarifa yake kwa wana Simba,
Mbunge huyo wa Tabora Mjini alisema amelazimika kuingilia kati suala
hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka
Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa Vitalo, klabu waliyotoka
wachezaji hao hawakuwa mjni na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba.
"Kila walipokuwa wakipigiwa simu kwa takribani siku tatu
mfululizo walikuwa wakisema kwamba wako milimani. Sasa hawa watu wa
Burundi wakikwambia wako miliman wanamaanisha wameenda kijijini kwao.
Kuongea kwa simu pekee kusingetosha na ndiyo Kamati ya Utendaji ya Simba
iliomba niende mwenyewe Burundi ili suala hili liishe," alisema.
Hii
ni mara ya pili kwa Rage, ambaye ana uzoefu wa kuongoza soka kwa zaidi
ya miongo mitatu, kuingilia kati suala la uhamisho wa wachezaji wa
kimataifa. Miaka miwili iliyopita, Mwenyekiti huyo alilazimika pia
kusafiri kwenda nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kushughulikia uhamisho
wa mchezaji Gervais Kago ambao nao ulikuwa na matatizo.
Kutokana
na kupatikana kwa ITC hizo, Kaze na Tambwe sasa wataruhusiwa kucheza
katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya JKT OIljoro ya Arusha iliyopangwa
kufanyika Jumatano ijayo mjini Arusha. Klabu ya Simba tayari imewakatia
wachezaji hao vibali vya kufanya kazi hapa nchini.
Wachezaji
wengine wa kigeni wa Simba, Joeph Owino na Abel Dhaira, walicheza
katika mechi ya jana kutokana na kukamilisha taratibu zote za uhamisho
na kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini.

0 Comments