Fraizer
Campbell alifunga mabao mawili ya Cardiff katika dakika ya 79 na 87 na kusababisha timu yake hiyo iliyo panda daraja msimu huu, kuondoka na pointi tatu muhimu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Cardiff City Stadium,na kuwapa ushindi wao wa kwanza msimu huu katika ligi kuu England na kuwaacha wakongwe wa Manchester City wasiamini kilichotokea.
![]() |
| Wanaweza kusonga mbele: Frazier Campbell alifunga mara mbili kwa upande wa Cardif City |
Timu hizo zote mbili zilimaliza kipindi cha kwanza zikiwa hazija fungana,lakini katika kipindi cha pili walioanza kushinda walikuwa
ni Manchester city kupitia kwa Edin Dzeko ndani ya dakika ya 52,baada ya kuachia shuti kali lililopita kati kati ya mabeki wawili wa Cardiff City na kupita juu ya mikona ya kipa,na hivyo kuiandikia bao la kwanza Manchester City.
Katika dakika ya 60, mchezaji wa Cardiff City
Aron Gunnarsson alisawazisha bao hilo na kuufanya ubao kusomeka moja moja,kisha Fraizer Campbell katika dakika ya 79 na 87 akaipatia bao la pili, na la tatu ambalo ndilo la ushindi kwa Cardiff City.
![]() |
| Fraizer Campbell alifunga katika dakika ya 79 na 87 |
![]() |
| Shujaa:Fraizer Campbell inawezekana akaweza kuthibitisha muhimu wake katika msimu wote,ndani ya timu hii iliyopanda daraja. |
Dakika za mwishoni kabisa yaani katika dakika ya 90,
Alvaro Negredo aliipatia bao la pili Manchester City,na huo ndio ukawa mwisho wa mchezo kwani baada ya dakika kadhaa refa alipuliza kipenga kuashilia mpira umekwisha.
![]() |
| Alvaro Negredo akifunga bao la mwisho la Manchester City |
![]() |
| Wakati wa kusherehekea: Mashabiki wa Cardiff wakisheherekea bao la Campbell |
![]() |
| Machester City wanakata tamaa |
![]() |
| Shujaa Campbell akiruka juu kushangilia |
Kikosi cha Cardiff City: Marshall 6;
Connolly 6, Caulker 7, Turner 7, Taylor 6; Bellamy 6 (Cowie,83mins),
Gunnarsson 7, Kim 7 (Mutch, 90mins), Medel 7, Whittingham 6; Campbell 8
(Cornelius, 90mins)
Akiba wasiotumika: Lewis, Hudson, Noone, Maynard
wafungaji: Gunnarsson 60, Campbell 79, 87
Kikosi cha Manchester City:
Hart 7; Zabaleta 4, Garcia 4, Lescott 5, Clichy 6; Navas 6 (Nasri,
55mins 5), Fernandinho 6 (Milner, 77mins 5), Toure 6, Silva 7; Aguero 6,
Dzeko 7 (Negredo, 69mins 6)
Akiba wasiotumika: Pantilimon, Kolarov, Nastasic, Rodwell
Wafungaji: Dzeko 52, Negredo 90
Refa: Lee Probert
Jumla ya waliohudhulia: 27, 068









0 Comments