Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:STARS SASA "RUKSA"MSIKILIZE RAIS ALI HASSAN MWINYI AKIFUTA KAULI YA "TANZANIA KICHWA CHA MWANDAWAZIMU KATIKA SOKA"

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.21,2015 SAA 01:23 USIKU

Rais wa awamu ya Pili wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi,amewakosha Watanzania na kuwapa moyo
zaidi baada ya kufuta kauli yake ile ya Usemi kwamba (Tanzania ni Kichwa cha Mwandawazimu katika soka),na Hayo ameyazungumza wakati akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio Efm ya Jijini Dar es salaam.
Ali Hassan Mwinyi akiwa na mtangazaji wa kipindi cha michezo Maulid Kitenge

Kauli hiyo ambayo wengi wanaamini kuwa ina ukweli juu yake,kwa kufananisha na matokeo ambayo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imekuwa ikiyapata katika michezo yake hivi karibuni.

"Kabisa,Sio hii ya Sasa,ile ya zamani ilikuwa mbali,sasa wamejifunza vijana na wamepata mafunzo mazuri na wanasikia maneno ya makocha wao,kwa hiyo hapana shaka na kila la Kheri nawatakia,na wataipata kila la Kheri wasiwe na wasiwasi wowote"alisema mzee "Ruksa" Ali Hassan Mwinyi alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hiko Maulid Kitenge kuwa kama rasmi ameifuta kauli yake kuwa Tanzania kichwa cha mwendawazimu katika soka ?.

MSIKILIZE  ALI HASSAN MWINYI AKIZUNGUMZA
 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments