Ticker

6/recent/ticker-posts

EXCLUSIVE:GARETH BALE AVUNJA REKODI YA DUNIA,AJIUNGA RASMI NA REAL MADRID KWA KITITA CHA £ 86MILLION

 Na.Herman Kihwili,IMEWEKWA AGOSTI 26,2013 SAA 09:00 alfajili
Kama ilivyo ada Blog ya Jamii na Michezo kukupa habali za ukweli na zilizotoka katika mda muafaka au siku hizi wanaziita habari zilizo vunjika au kwa lugha ya kimombo wanaziita Breaking News,sasa tunawaletea hii,baada ya siku ya jana muda kama huu blog hii kuandika,"inatarajiwa ndani ya maasa 24 yajayo mchezaji huyo,hatma yake itakuwa imejulikana".
Mchezaji wa Ghali sana duniani: Daniel Levy  hatimaye amekubaliana  na Real Madrid
Hatimaye hayawi hayawi sasa yamekuwa,kwani sasa Gareth Bale yuko huru kujiunga na  Real Madrid baada ya kukubaliana na 
Tottenham kutoa mkwanja  uliovunja  rekodi ya dunia  wa £ 86million,na makubaliano hayo yamefanyika  siku ya Jumapili usiku.
Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesaini makubaliano ya kuachana na mchezaji huyo ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wa PFA kufuatia mazungumzo na wakurugenzi wa jopo la viungozi ndani ya White Hart Lane. 
Maisha ndani ya Hispania: Bale alicheza  mechi moja tu katika michezo ya kujiandaa na  kabla ya msimu na timu yake ya Spurs
Uhamisho bale kwenda Real,unapindua rekodi ya dunia ya £80m  ambayo ililipwa kwa Manchester United,kwa ajili ya Cristiano Ronaldo mnamo mwaka 2009.
Levy alipomaliza mazungumzo na Madrid pamoja na wakala wa Bale,Jonathan Barnett na mkurugenza wa Tottenham wa bechi la ufundi Franco Baldini alienda kuangalia klabu yake ambayo ilishinda 1-0 dhidi ya Swansea City baada ya kukubaliana na mpango huo.  
Na inaeleweka kwamba uamuzi wa kusafiri kwenda Madrid kukutana na Perez - ambaye anajua hali harisi,ni mbinu tu iliyoundwa ya  kupata bei ya juu.

Anakutana na hawa:Bale anajiunga na  timu ya Real Madrid na anatarajiwa kutambulishwa siku ya jumanne
Ada hii imerudisha faida kubwa na ya ajabu kwani mchezaji huyo alijiunga na  Spurs  kwa kiasi cha £ 7m kutoka klabu ya Southampton miaka sita iliyopita na pia imeongeza sifa kwa  Daniel Levy kiongozi aliye tukuka katika mchezo.
lakini pia unakuwa uhamisho mkubwa na uliochukuwa muda mrefu na wa kihistoria kuwahi kutokea katika mchezo,kufuatia mazungumzo ndani ya majira haya ya joto.

Post a Comment

0 Comments