Ticker

6/recent/ticker-posts

MANUEL PELLEGRINI NA ROBERTO MARTINEZ,WAWAPIGIA CHABO MANCHESTER UNITED NA CHELSEA


 

Kocha mpya wa Evaton Roberto Martinez  sambamba  kocha wa Man City Manuel Pellegrini,walionekana wakiupigia chabo  mchezo kati ya timu ya Manchester United na Chelsea ambao
walitoka sare ya bila kufungana katika mchezo uliopingwa katika uwanja wa Manchester United wa  Old Trafford,kwania ya kupata mbinu mbadala ili timu zao zitakapokutana basi wajue wapi pa kuanzia.
Wayne Rooney atauzwa kweli kwa mchezo aliouonyesha jana?
Lakini katika mchezo huo ingawa United walinyesha mchezo mzuri chini ya kocha wao mpya David Moyes aliyechukuwa mikoba ya Sir Alex Ferguson, ulikuwa ndio mchezo wake wa kwanza kukutana na Chelsea akiwa kama kocha wa United,lakini hakuweza kufua dafu katika mchezo huo wa ligi kuu japo walikuwa nyumbani,walikosa nafasi nyingi tu,lakini Wayne Rooney,kwa upande wa United alionesha kiwango cha juu katika mchezo huo.
Mtumzima yuko kikazi zaidi
Mchezaji huyo ambaye ana husishwa kutakiwa na klabu ya Chelsea, bila shaka klabu hiyo itakuwa na nafasi adimu ya kuweza kumnunua kwa kuwa haidhaniwi klabu ya Manchestar United inaweza kuwauzia jembe alafu wao wakabaki mikono mitupu kama walivyofanya Arsenal kwa Van Persie.


Kwa upande wa Chelsea,mchezaji mpya aliyesajiliwa katika msimu huu,Andre Schurrle kiukweli alionyesha mchezo mzuri japokuwa alitolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Azpilicueta.

Mpira umegusa mkono : Inaaminika hii iliuwa penalti baada ya mpira kugonga mkono  wa Lampard

Kikosi cha Man United: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia (Young 67), Cleverley, Carrick, Welbeck (Giggs 78), Rooney, Van Persie.
Wachezaji wa akiba: Anderson, Smalling, Lindegaard, Kagawa, Buttner.
Kikosi cha Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne (Torres 60), Oscar, Hazard (Azpilicueta 93), Schurrle.
Wachezaji wa akiba: Essien, Mikel, Lukaku, Schwarzer, Mata.
Kadi za njano: De Bruyne, Torres.

Mbwatukaji:Kama kawaida yake kulalama

Upendo kwa mashabiki kidogo


amani na upendo

Post a Comment

0 Comments