Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA AGOSTI 25,2013 SAA 10:00 jioni
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Ashanti United
iliyochezwa jana (Agosti 24 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 102,856,000.
Watazamaji
17,744 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba moja ya VPL msimu
wa 2013/2014 iliyomalizika kwa
mabingwa watetezi Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.
mabingwa watetezi Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 24,400,102.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,689,898.31.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 12,406,831.75,
tiketi sh. 4,453,890, gharama za mechi sh. 7,444,099.05, Kamati ya Ligi
sh. 7,444,099.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,722,049.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,894,927.41.

0 Comments