Ticker

6/recent/ticker-posts

MWANA DADA BINGWA WA KURUKA VIUNZI DUNIANI,AKEMEA USHOGA.

 Bingwa wa dunia  wa mchezo wa kuruka viunzi,mwana dada Yelena Isinbayeva ameongelea ushoga michezoni, huku kukiwa na maandamano makubwa katika nchi yake ya asili ya Urusi  juu ya sheria mpya,ambapo kwa Sasa ni kinyume cha sheria kwa mtu menye umri  chini ya miaka 18 kutoa habari kuhusiana na  ushoga nchini Urusi.
Mwanadada Yelena Isinbayevana ni bingwa wa dunia wa kuruka viunzi
Lakini Yelena msimamo wake ni  kukosoa wanariadha ambao wanaunga mkono  mashoga na wasagaji.
"Tuna hofu sana kuhusu taifa letu kwa sababu wenyewe wanafikiria ni kawaida, " alisema Isinbayeva.

"Kila kitu huja kutokana na historia, Sisi kamwe hatukuwa  na matatizo haya katika  nchi yetu ya Urusi, na hatutaki kuwa nayo  katika siku zijazo,"aliongeza Isinbayeva,baada ya kushinda medali ya tatu ya dunia,siku ya jumanne. 
Tunaishi wavulana na wanawake au  wanawake na wavulana,na si vinginevyo:Anasema Yelena Isinbayeva
Msichana huyo  bingwa wa michezo ya riadha kutoka urusi,ambaye ana umri wa miaka 31, ana medali mbili za dhahabu za Olimpiki na  anashikilia rekodi  ya 28 duniani, pamoja na  mafanikio ya ubingwa wa Dunia,amekuwa maarufu na anapendwa sana katika nchi yake. 
Kiukweli ameonyesha kitu gani anaamini katika nafasi ya taifa lake juu ya maswala ya ushoga,na kusema kuwa  "tunaishi wavulana na wanawake au  wanawake na wavulana,na si vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments