Arsenal bado hawajakata tamaa katika jitihada za kumnasa nyota wa Liverpool Luis Suarez,baada ya kuongeza ofa nyingine ya £ 49 kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji huyo,ambaye amekuwa na mzozo na klabu ya juu ya hatma yake.
Mmiliki wa klabu hiyo, John W Henry, tayari amekataa ofa mbili ya £
35 milioni na £ 40 milioni kutoka kwa Arsenal, na ameahidi kwamba Suárez hauzwi kwa makubaliano yeyote kwenda Arsenal msimu huu.
![]() |
| Anatolewa macho:Luis Suarez amekuwa akiichanganya klabu yake ya Liverpool,na Arsenal wanatumia fursa ya kumshawishi |
Suárez alinukuliwa na gazeti la Jumatano la nchini Uruguayan linaloitwa El Observador akisema kwamba kwa sasa wameamua kubaki katika klabu ya Liverpool kwa sababu ya upendo wa mashabiki, lakini baada ya mechi kati ya timu yake ya taifa la Urugwai ambapo walishinda 4-2 dhidi ya Japan,alipozungumza na waandishi wa habari akakanusha,na kusema taharifa hizo si za kweli.
Mshambuliaji huyo Amekuwa akifanya mazoezi ya klabu peke yake,kufuatia mahojiano na The Daily Telegraph wiki iliyopita,Suarez ali mshitakiwa meneja wake Brendan Rodgers kwamba ameenda kinyume na ahadi walizokubaliana msimu uliopita, kwamba angeweza kuondoka ikiwa klabu ikashindwa kufuzu kwa katika Ligi ya Mabingwa.lakini kocha Rodgers amesema kuwa Suárez lazima aombe msamaha kwa kauli yake hiyo kama anataka kucheza tena Liverpool,kwa kuwa hakukua na makubaliano yeyote.

0 Comments