Uongozi wa klabu ya yanga ya jijini Dar es salaam,umesema kitendo
walichokifanya wachezaji wake wawili wa zamani Stephano Mwasika pamoja na
Shedrack Nsajigwa kuandika barua ya malalamiko ya kutolipwa fedha zao na
kuipeleka katika shilikisho la soka nchini, ni kuizalilisha klabu hiyo.
![]() |
| katibu mkuu wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako,akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo |
Akizungumza leo hii,katibu mkuu wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako,amesema klabu ya yanga haina nia mbaya ya
kutokuwalipa wachezaji hao,lakini inakiri kuwachelewesha pesa za wachezaji hao,lakini klabu hiyo imesikitishwa na wachezaji hao,kupeleka malalamiko katika shilikisho la soka nchi.
Aidha Mwalusako ameongeza kuwa,walipanga kukaa kikao na wachezaji hao siku ya tarehe 20 mwezi huu,lakini ikashindikana,kwa sababu ya mawasiliano,lakini klabu hiyo imesema itapanga tarehe ya kukutana na wachezaji hao ili waweze kuyamaliza maswala hayo.
Stephano Mwasika pamoja na Shedrack Nsajigwa ,wanadai klabu hiyo jumla ya shilingi milioni 16,ambapo Nsajigwa yeye anadai shilingi milioni 10 na Mwasika anadai klabu hiyo kiasi cha shilingi milioni 6.
Uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Twga na jangwani,umewataka wachezaji hao kutokuwa na wasiwasi,kwani kila kitu kitakwenda sawa.

0 Comments