Tiketi
kwa ajili ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil zitaanzwa kuuzwa siku ya Jumanne,lakini blog ya Jamii na Michezo inatambua kuwa hata wewe msomaji wa blog hii unao uwezo wakununua tiketi hizo kwa njia ya tovuti ya FIFA.
Karibu
na tiketi 3.3million zitakuwa zinapatikana kwa ajili ya
mashindano,
gharama ni kati ya £ 58 na £ 632 kwa bei ya mwisho katika uwanja wa
Maracana mjini Rio.
Kuna
mechi 64 katika mashindano na FIFA wana imani kutakuwa na mahitaji sawa na wao katika Kombe la Dunia la mwaka 2006 nchini Ujerumani.
![]() |
| Itajirudia? Wayne Rooney pichani akiipatia bao timu yake ya taifa la England dhidi ya Brazil katika uwanja wa Maracana |
Maombi
tayari yameshaanza kutumwa katika tovuti ya FIFA,na inasemekena kuwa kuna foleni kutokana na mahitaji kuwa mengi mno kupita kiasi kwa ajili ya kupata tiketi.
"daima itakuwa ni vigumu kutabiri,"Mkurigenzi wa masoko wa FIFA Thierry Weil,aliongea na BBC.
"Lakini Ninaamini kuwa itakuwa ni zaidi kile kilichotokea katika nchi ya Ujerumani na zaidi ya kilichotokea nchini Afrika Kusini mwaka 2010."


0 Comments