Ticker

6/recent/ticker-posts

ROBERT LEWANDOWSKI,AMALIZANA NA BORUSSIA DORTMUND

 IMEWEKWA AGOSTI 21,2013 SAA 11:37 JIONI
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski imeamua kuweka kando tofauti zake  na klabu yake,juu ya uhamisho alioshindikana wa Bayern Munich katika msimu wa hivi karibu,mchezaji huyo wa  kimataifa Poland aliyasema hayo hii.
Kesi imekwisha sasa
Lewandowski ilikuwa ameshakata tamaa na kutaka kuondoka katika klabu hiyo na kijiunga na maasimu wa klabu hiyo Bayern
Munich lakini mpango huo ukashindikana  baada Dortmund
kugomea  uhamisho huo, ikisema kuwa mchezaji huyo alikuwa na mkataba  hadi  mwaka 2014.
Vita kali ya maneno ilitokea baina ya pande hizo mbili, kuongeza wasiwasi juu ya hatma ya mchezaji huyo ndani ya  Dortmund katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake.
"Hali  ya sasa ni kwamba mimi nitakaa Dortmund kwa mwaka mmoja zaidi," alisema Lewandowski akiliambia gazeti la michezo la  Bild.  
"Tumeweza kuweka kando tofauti zetu zote na tumeweka kila kitu sawa, Kweli kulikuwa na makosa lakini,tayari tumemaliza kila kitu na ( kesi) mjadala umefungwa tayari." aliongeza Mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski.

Post a Comment

0 Comments