Ticker

6/recent/ticker-posts

ARSENAL,HAWAKULALA USIKU WA KUAMKIA LEO,WAFANYIWA VURUGU KABLA YA MECHI DHIDI YA FENERBAHCE

Maneja wa Arsenal Arsene Wenger,alizani kwamba angekuwa na usingizi mzuri usiku wa kuamkia hii leo,akifikilia mechi dhidi ya Fenerbahce ya Uturuki,lakini inonekana ilikuwa tofauti juu ya mawazo ya mashabiki wa  Fenerbahce ya Uturuki.
Arsene Wenger:Atatoka leo baada ya kukosa usingizi?
  Jamii na Michezo inasema hivyo kwa sababu,usiku wa kuamkia
leo, timu hiyo ya Arsenal imefanyiwa fitna za kimchezo na mashabiki watukutu na wasiokuwa na adabu  wa timu hiyo ya uturuki,baada ya kuwapigia kelele kwa kuimba nyimbo zisizokuwa na maana usiku kutwa,nje ya hoteli waliofikia timu hiyo ya Arsenal.
 
Hakuna kulala,ni kukesha tu.
Mashabiki hao wa timu ya hiyo ya Uturuki waliwasha moto au kwa jina la kimombo (fireworks) zinazotumika wakati wa sherehe,na kumfanya meneja huyo,kutopata usingizi kabisa.

FITNA SIO AFRIKA TU,HATA KWA WENZETU ZIPO PIA 
Tuache hayo msomaji wa blog hii ya Jamii na Michezo tuangalie kidogo mchezo wa leo ambapo klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza inajitupa uwanjani jioni huu kumenyana na Fenerbahce ya Uturuki,lakini  katika mchezo huo Arsenal itakosa huduma ya kiungo wake wa kati Alex Oxlade-Chamberlain baada ya kupata jeraha la goti wakati wa mchuano wa ligi kuu nchini Uingereza siku ya Jumamosi iliyoita dhidi ya Aston Villa.

 Kocha Arsenal Wenger atawategemea mabeki kama Bacary Sagna, Kieran Gibbs na Nacho Monreal kushikilia ngome ya Arsenal watakapokuwa nchini uturuki leo hii.
Fenarbahce inashiriki katika michuano hii wakati ikisubiri matokeo ya rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la soka barani Ulaya baada ya kufungiwa nje ya mashindano haya kwa kosa la kupanga matokeo.
Rufaa hiyo itaamuliwa tarehe 28 siku moja baada ya mchuano wa muaridano na Arsenal ugenini.
Arsenal ina rekodi nzuri ya kufuzu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kufanya hivyo kwa misimu 15 iliyopita.


Post a Comment

0 Comments