Ticker

6/recent/ticker-posts

IVANOVIC,AIOKOA CHELSEA KUEPUKANA NA SARE,YAICHAPA ASTON VILLA BAO 2 KWA 1

Kipindi cha Jose Mourinho akiwa  na wasiwawasi,hakika kila mtu atajua kuhusu hilo, wachezaji, viongozi na mashabiki 40,000  ndani ya Stamford Bridge watashuhudia tukio hilo.Na hayo yameshuhudiwa hapo jana,baada ya timu ya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Aston villa

Eden Hazardakishangilia bao la kwanza la Chelsea lililosababishwa na yeye,lakini limefungwa na mchezaji wa Aston Villa Antonio Luna.   

Point tatu muhumu:Chelsea wakisheherekea baada ya ushindi

Bao la kwanza la Chelsea lilipatikana baada ya mchezaji wa timu ya Aston villa Antonio luna kujifunga mwenyewe kwa bahati mbaya katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Eden Hazard dakika ya 6 tu ya kipindi cha kwanza,lakini goli hilo lilisawazishwa katika dakika ya 45 na Mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke.

Christian Benteke akisheherekea baada ya kusawazisha bao la kwanza klabla ya Chelsea kuibuka na ushindi,na chini kocha  bosi wa Villa Paulo Lambert,ikishangilia bao hilo
    
Nguvu zaidi inatumika:Ivanovic akionyesha ishara ya ushindi

Alikuwa ni Branislav Ivanovic ndiye aliyeiwezesha Chelsea kuweza kumfanya Jose Mourinho na mashabiki  kuondoka na furaha baada ya kupata goli safi kwa kichwa ndani ya dakika 73 na kuweka wasiwasi kando baada ya dakika 90 kukamilika.

Jose Mourinho muda mwingi alikuwa akizozana na
Paulo Lambert


kikosi cha Chelsea: Cech 7, Ivanovic 6, 7 Cahill, Terry 8, Cole 6, Ramires 6, Lampard 6, Oscar 6 (van Ginkel 84), Mata 6 (Schurrle 65), UN ya 7, Ba 4 (Lukaku 65).

AKIBA: Mikel, De Bruyne, Schwarzer, Azpilicueta.
KADI: Ivanovic

wafungaji: Luna (og) 7, Ivanovic 73.

kikosi cha Aston Villa: Guzan 6, Lowton 6, Vlaar 7, Clark 6 (Okore 43), Luna 7, El Ahmadi 7 (Tonev 82), Westwood 7, Delph 7, Weimann 6, Benteke 7, Agbonlahor 7.

AKIBA: Bennt, Bacuna, Helenius, Bad, Sylla.

KADI: El Ahmadi, Westwood, Benteke

mfungaji: Benteke 45

Mahudhurio: 41,527

Mwamuzi: Kevin Friend

Macho juu ya mpira:  Ivanovic  karibu na Benteke

Post a Comment

0 Comments