Licha ya timu ya Arsenal kufanyiwa fitna za kimchezo na
mashabiki watukutu na wasiokuwa na adabu wa timu hiyo ya Fenerbahce ya uturuki,baada
ya kuwapigia kelele kwa kuimba nyimbo zisizokuwa na maana usiku kucha wa kuamkia jana,nje ya hoteli waliofikia timu hiyo ya Arsenal,lakini timu ya Arsenal imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3 kwa o dhidi ya majitu hayo ya kituruki usiku wa kuamkia hii leo.
![]() |
| Furaha:Carl Jenkinson, Kieran Gibbs, Theo Walcott, Aaron Ramsey and Olivier Giroud wakisheherekea ushindi |
Magoli yote matatu yalifungwa ndani ya kipindi cha pili, na alikuwa ni Kieran Gibbs ndiye aliyekuwa wa kwanza kabisa kuliona
lango la Fenerbahce katika dakika ya 51,kabla ya Aaron Ramsey kuipatia Arsenal bao la pili bada ya kuachia shuti kali katika dakika ya 64 lililomshinda kipa wa Fenerbahc,na hivyo kuingia moja kwa moja nyavuni,bao la tatu la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 77. ![]() |
| Hakuna kosa: Olivier Giroud akipiga penalt ya adhabu baada ya Walcott Theo kufanyiwa makosa na Mikali Kadlec katika box |
![]() |
| Muonekano wa mafaniko:Wenger ameanza vizuri kampeni za ligi ya mabingwa |
![]() |
| Refaaa! huonii? |
Mchezaji Laurent Koscielny hakumaliza mchezo baada ya kutolewa kutokana na maumivu baada ya kupasuka karibu na jicho baada ya
kupigwa buti na Pierre Webo.
Fenarbahce inashiriki katika michuano hii wakati ikisubiri matokeo ya
rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la soka barani Ulaya baada ya
kufungiwa nje ya mashindano haya kwa kosa la kupanga matokeo.
Rufaa hiyo itaamuliwa tarehe 28 siku moja baada ya mchuano wa muaridano na Arsenal ugenini.
![]() |
| Mguu juu: Koscieln,akipigwa boot na Webo katika uso |
![]() |
| Koscielny alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Carl JENKINSON |
kikosi cha Fenerbahce:
Demirel 5, Irtegun 4 (Gonul 46, 5), Yobo 6, Bruno Alves 6, Kadlec 5,
Topal 5, Meireles 6 (Potuk 82), Emre 6, Sow 4, Webo 4 (Emenike 62, 5),
Kuyt . 5
wachezaji wa akiba wasiotumika: Gunok, KORKMAZ, Baroni, Erkin.
KADI za njano: Webo, Alves, Kadlec.
![]() |
| Hisia za kuchanganjikiwa: Bacary Sagna na Mertesacker wakipeana tano na kuondoka, lakini Mousa Sow hawezi kuamini macho yake kilichotokea |
kikosi cha Arsenal. Szczesny 7, Sagna 7, Mertesacker 7, Koscielny 6 (JENKINSON 33, 6), Gibbs 7, Rosicky 7, Wilshere 6, Ramsey 8, Cazorla 6, Giroud 6, Walcott 7 (Monreal 87)
wachezaji wa akiba wasiotumika: Fabianski , Podolski, Sanogo, Frimpong, Gnabry.
KADI za njano: Szczesny.
wafungaji: Gibbs 51, Ramsey 64, Giroud (kalamu) 77.
Mwamuzi: Gianluca Rocchi (Italia)
Walihudhuria: 50,500.







0 Comments