Na. Baraka Kizuguto,pamoja na Herman Kihwili
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda anayechezea klabu ya Young Africans Hamis Friday Kiiza 'Diego' kesho jioni anatarajia kusafiri kuelekea nchini Lebano kufanya majaribio ya wiki moja katika klabu ya Al Ahed SC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda anayechezea klabu ya Young Africans Hamis Friday Kiiza 'Diego' kesho jioni anatarajia kusafiri kuelekea nchini Lebano kufanya majaribio ya wiki moja katika klabu ya Al Ahed SC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Kiiza ambaye mpaka sasa ameshaitumikia Young Africans kwa miaka
miwili, aliongeza mkataba wa miaka miwili tena kuitumika klabu yenye
maskani yake twiga/jangwani kufuatia kumalizika kwa
mkataba wa awali ambapo sasa mkataba wake utamalizika mwaka 2015.
mkataba wa awali ambapo sasa mkataba wake utamalizika mwaka 2015.
Al Ahed SC
Mabingwa mara tatu (3) wa kombe la Ligi Kuu nchini Lebanon, washindi
mara nne (4) wa kombe la FA na washiriki wa kombe la Vilabu Bingwa
barani Asia mara sita (6) wamekamilisha taratibu zote kwa ajili ya
mchezaji kwenda kufanya majaribio.
Hamis Kiiza ataondoka kesho
jioni kwa shirika la Ndege la Ethiopia ambapo ataanza mazoezi kwa siku
saba (7) kuanzia alhamisi tarehe 22.08.2013 na anatajiwa kurejea nchini
mwisho wa mwezi Agosti 31, 2013.
Wakati huo huo kikosi cha
mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013 na mabingwa wa Ngao ya Hisani
2013/2014 leo wameendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya
sekondari Loyola kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa VPL dhidi ya Ashanti
United siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa jini Dar es
salaam.
Katika mchezo dhidi ya Azam kugombea Ngao ya Jamii
wachezaji Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na Ally Mustapha 'Barthez;
walipata majeraha kufuatia kuumizwa na washambuliaji wa Azam John Bocco,
Gaudence Mwaikimba na Kipre Tchetche hali zao zinaendelea vizuri.
"Leo
wamefanya mazoezi mepesi isipokuwa Kelvin Yondani aliyepewa mapumziko
na daktari kwa siku tatu (3) kufuatia kupatiwa matibabu ya nyama ya paja
aliyoumia siku ya mchezo huo na anatajiwa kurejea dimbani siku ya
jumatano kuungana na wachezaji wenzake katika mazoezi" alisema Dr
Matuzya.
Young Africans inajiandaa na mchezo dhidi ya Ashanti
United siku ya jumamosi tarehe 24.08.2013 utakaofanyika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom
msimu wa 2013/2014.

0 Comments