Ticker

6/recent/ticker-posts

TAHARIFA KUHUSIANA NA KESI YA OSCAR PISTORIUS.

 Na.Deutsche Welle
 
Bingwa wa mbio za Olimpiki kwa Watu Wenye Ulemavu Duniani, Oscar Pistorius  atafikishwa mahakamani mwezi wa Machi
mwakani kujibu mashtaka ya kumuua mpenzi wake wa kike katika Siku ya Wapendanao. Raia huyo wa Afrika ya Kusini mwenye umri wa miaka 26 ambaye hana miguu yote miwili alikuweko mahakamani leo hii wakati uamuzi huo ukitolewa na anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia. Pistorius amerudi tena kizimbani ikiwa ni miezi sita baada ya kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake Steenkamp katika choo cha nyumba yake ilioko Pretoria alfajiri ya tarehe 14 mwezi wa Februari. Mwanariadha huyo hivi sasa yuko nje kwa dhamana na alikiri kumuuwa mpenzi wake huyo lakini amekanusha kwamba alifanya hivyo kwa kukusudia akisema kwamba alimpiga risai kupitia mlango wa choo uliokuwa umefungwa kwa kumdhania kuwa ni mwizi. Kesi hiyo ilisikilizwa kwa muda mfupi leo hii kwa sababu mawakili walikuwa tayari wamekubaliana kuanza kusikiliza kesi hiyo mwakani kutokana na mzigo mkubwa wa kesi unaozikabili mahakama za Afrika ya Kusini.

Post a Comment

0 Comments